HATUA YA 14; UNA NGUVU NDANI YAKO.

Una nguvu kubwa sana ndani yako. Inawezekana hujawahi kuambiwa hata siku moja. Leo ninakwambia ipo nguvu ndani yako ya kushinda yote ambayo unayapitia sasa. Ipo ngvuvu ndani yako ya kukuwezesha kufikia yale yote unayoyataka. Haijalishi sasa hivi unaona giza. Au unapitia magumu kiasi gani. Tumia uwezo ulio ndani yako kuzishinda changamoto unazopitia sasa. Una nguvu […]

HATUA YA 13; Ipo Siku.

Hapo zamani kabla ya kutambua ni kitu gani natakiwa kufanya ili nifikie Mafanikio nilizoea kusema ipo siku ndoto yangu itatimia. Ni maneno mazuri sana na ya kutia Moyo lakini kama hakuna unachofanya hiyo ndoto itabakia kuwa ndoto. Ipo siku utatambua haya ninayosema ni Kweli. Huwezi kusubiria mazao wakati hakuna shamba lolote ulilootesha mbegu. Ili neno […]

HATUA YA 12; Wewe Rafiki Yangu.

Wewe ni Rafiki Yangu hivyo lazima wakati wote niwe nakwambia Ukweli. Ukweli ni kwamba usipokubali kubadilika mwaka 2017 utakua mgumu zaidi. Wewe Rafiki Yangu usiopoacha kuishi maisha yako halisi utaishia kuteseka moyoni mwako kwa kuwaridhisha wengine. Wewe Rafiki yangu acha kuwa mzembe kila siku nakwambia kusoma vitabu ni muhimu sana lakini unahisi nakutania. Lakini ipo siku […]

HATUA YA 11; Furaha yako Inatoka Wapi?

Furaha yako inatoka wapi? Nataka ujiulize leo furaha yako inatokana na nini!  Kila mmoja ana jibu lake juu ya chanzo cha furaha yake. Kama furaha yako inaletwa na vitu au watu kuna wakati utakosa furaha. Wakati vitu havipo utakosa furaha, watu wakikuacha utakosa furaha. Kama furaha yako inaletwa na mali nyingi utaishi bila furaha hadi […]

HATUA YA 10; Tafuta sababu ya Tatizo

Kila kinachotokea Maishano mwako kinatokea Kwasababu.  Changamoto yeyote unayopitia ipo Kwasababu. Ugumu wa Maisha unaopitia upo Kwasababu. Ukosefu wa pesa ulionao upo Kwasababu. Kuachwa na umpendae imetokea Kwasababu. Kudharauliwa kumetokea Kwasababu. Kusemwa kunatokea Kwasababu. Hakuna kinachotokea kwa Bahati mbaya hata siku moja. Kuna sababu nyuma ya lolote linalotokea. Umefanikiwa Kwasababu ulifanya kazi kwa bidii. Badala […]

HATUA YA 9; Tabia ya Uvivu.

Tabia ya Uvivu ndio inasababisha wengi wanapata hasara ya maisha pamoja na matatizo mbalimbali.  Tabia ya Uvivu mara nyingi huletwa na kuridhika na kile unachokipata. Kama mtu ana uhakika wa kupokea laki nane kwa mwezi anajisahau kabisa kwamba hana umiliki na kazi yake. Badala ya kuongeza bidii na Kutafuta chanzo kingine cha mapato mtu huyu […]

HATUA YA 8; UADILIFU

Uadilifu ni kitu cha muhimu sana kwenye Maisha yetu ili kutuwezesha kujenga historia nzuri. Watu wengi wanakosa uadilifu ndio maana biashara zao zinakufa baada ya muda mfupi. Uadilifu ni sifa ambayo itakufungulia milango mingi ya fursa huko mbeleni. Kama utakosa uadilifu katika hatua hizi za mwanzo unaanza kuonyesha picha ya wewe ulivyo na  huko mbeleni […]

HATUA YA 7; Kurudia Rudia.

Kabla hujasema Haiwezekani umeshajaribu mara ngapi?  Kabla hujaamua kuacha umefanya kwa Kiwango cha kuridhisha? Umerudia mara ngapi? Hivi unajua kila mbegu ina muda wake wa kukaa chini? Kama mwaka jana ulipanda mahindi na hukuvuna kabisa Kwasababu ya uhaba wa mvua haiwezi kuwa mwisho wa kupanda mwaka huu.  Utatafuta namna nyingine. Tabia ya Kurudia Rudia anatakiwa […]

HATUA YA 6; Nidhamu

Nidhamu ndio kitu cha muhimu sana katika safari yetu ya Mafanikio. Nidhamu ni pale unapoamua kufanya kitu iwe unataka au hutaki. Kama umesema utasoma vitabu viwili kwa mwezi usome kwa namna yeyote ile. Nidhamu ndio inaweza kukufanya ujijengee tabia mbalimbali nzuri za Mafanikio. Kama mimi nilipoamua kuandika makala hizi za kukutia moyo na kukushauri. Haijalishi […]

HATUA YA 5; Enjoy the Journey.

Mafanikio ni safari na safari yeyote ina changamoto zake. Usione wanaopanda ndege ufikiri huwa nyakati zote ni furaha tu. Kuna wakati ndege hupata misukosuko angani pia. Misukosuko yeyote unayopitia tambua ni safari huwa zipo hivyo. Ukifika wakati wa kula safarini wewe kula,  Ukifika wakati mnatakiwa mpumzike pumzika. Bahati mbaya sana hili gari la Mafanikio unaendesha […]